Jengo la utawala la shule ya Wasichana Iringa iliyopo kata ya Kihesa, Jimbo la Iringa mjini, Manispaa ya Iringa Mkoa wa Iringa. Shule
hii ni moja shule ya maalumu nchini Tanzania inayolea watoto wenye
ulemavu wa ngozi na viungo pamoja na wale wasio sikia na kuona, licha
yakuwa na uhaba wa walimu wakuwawezesha walemavu hawa kwa mfano vipofu
na viziwi, shule hii imekuwa ni moja ya shule ambazo zimeweza
kuwasaidia kuwalea kimwili, kisaikolojia na kiakili.
Moja ya maabara inayotumika kwa masomo ya sayansi yaani somo la biolojia, fizikia na kemia katika shule ya Sekondari ya Wasichana ya Iringa.
Maktaba ya shule ya sekondari ya wasichana ya Iringa iliyosheni vitabu licha ya changamoto zilizopo
ikizihirisha ni kivipi wadau wa elimu pamoja na serikali, viongozi wa serikali ambavyo wamelitupia macho suala la maktaba licha yakuwa vitabu vilivyo vingi haviendani na elimu ya mazingira yetu ya Tanzania na viwango vya elimu ya kidato cha kwanza mpaka cha sita.
Kuna umuhimu wa serikali na wadau wa elimu kuiangalia shule hii kwa jicho la tatu kwa kuiboresha maktaba
hii kwa kuongeza vitabu vinavyoendana na elimu ya mazingira na mtaala wetu na kuboresha miundombinu ya maktaba ili kuweza
kuwavutia wasomaji na watumiaji wa maktaba.
Moja ya majengo ya madarasa yanayotumika katika shule ya sekondari ya wasichana Iringa
Mazingira ya shule ya sekondari ya wasichana ya Iringa yaliyojawa na miti ya maua na vivuli kwa ajili ya kupumzikia pamoja na hewa safi. |